Tuesday, June 25, 2013

Jeshi la Polisi lazungumza kuhusiana Joyce Kiria kutokujua aliko mumewe, Henry Kilewo.


“Hapa ni karibu kabisa ya ukumbi wa habari maelezo ambapo niliwafuata waandishi wa habari ili kupata muda wa kuongea nao, nikiwa nimewabeba wanangu Lincon na Linston.”


Mwishoni mwa wiki ziliripotiwa taarifa za kukamatwa kwa makada wa CHADEMA akiwamo Henry Kilewo mumewe Joyce Kiria (mwenye kipindi cha “Wanawake Live” katika kituo cha runinga cha EATv), ambaye katika ukurasa wake wa Facebook, aliandika kuwa hafahamu alikopelekwa mumewe baada ya kumkosa alipompelekea chaukula katika kituo cha polisi alipokuwa anashikiliwa.

Henry Kilewo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza."



Msemaji wa jeshi la Polisi nchini Tanzania, Advera Senso amesema:

Inasikitisha kuona kwamba huyu mama Joyce Kiria anaingilia mambo ya kisheria na kutaka kupotosha jamii kwamba hajui mume wake yuko wapi pia nadhani analenga kuichochea jamii kwamba aliyetuhumiwa kutenda uhalifu akikamatwa familia yake iandamane, tendo ambalo pia ni kosa la jinai.

Aidha anatakiwa kuheshimu haki za watoto na kuacha kuwatumia katika kinga ya kutetea watu wanaotenda uhalifu.


Kwenye blog-site yake ya joycekiria.com Joyce ameweka picha na kuandika yafuatayo:

NAOMBA MSAADA KWA RAISI WANGU WA NCHI, IGP SAID MWEMA, WANAWAKE WENZANGU NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA.

NAOMBA MSAADA KWA RAISI, IGP MWEMA NA WANANCHI WOTE NIPATE HAKI ZANGU NIKIWA KAMA MAMA NA MKE KUFAHAMU KUJUA MUME WANGU ALIPO.

Baada ya kukaa kwa siku mbili bila kujua alipo mume wangu, nimejitokeza mbele ya waandishi wa habari wapate kunisaidia kufikisha ujumbe wangu wa kupata msaada ya kujua mume wangu alipo.

Nina watoto wawili mkubwa ni wa miaka 2 na mdogo wake ni wa miezi 4, leo ni siku ya nne hawajamuona baba yao, baba yao ni msaada mkubwa mno kwa familia yangu, Raisi Kikwete huko ulipo nakuomba usikie kilio changu, IGP Said Mwema nahitaji msaada wako, Wanawake na Wote nahitaji msaada wenu.

...kutopewa taarifa ya mume wangu halipo. Sina Amani kabisa naomba kupata taarifa kamili huko aliko yuko salama? na hata kufahamu anakula nini?

Kubwa watanzania wenzangu ni kunisaidia katika maombi ili huko aliko awe salama.

Kwa Urefu zaidi habari hii itaruka katika vyombo mbalimbali vya habari zikiwepo TV kama Channel Ten, ITV, EATV, Star TV na Clouds, Radio kama Clouds, Radio One, na magazeti kama Mwananchi, Nipashe , Mtanzania, Tanzania Daima , The Citizen, Guardian, na vyombo vingine vya habari.

Nawashukuru waandishi wote ambao walikuwepo hapa, pia na watanzania wote naamini mko pamoja na mimi.

No comments:

Post a Comment